Tanzania Newsletter September 2013 – Swahili

 
Utangulizi

IDC Ltd ni mkusanyiko wa wataalamu washauri katika maendeleo endelevu. Tumebobea katika tafiti za kijamii na kiuchumi, Tathimini za athari (ESHIAs), uandaaji wa sera, usimamizi wa utekelezaji, mpango wa makazi mapya (RAPs), Maudhui ya wenyeji na maendeleo ya shughuli za kiuchumi. Tunatumia njia za kibunifu katika kutafuta ufumbuzi wa kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Ingawa tumejikita zaidi Afrika kazi zetu zimeenea kimataifa. Utendaji wa kazi za IDC Ltd unazingatia kuwa endelevu. Tunajenga uwezo wa vijana wahitimu wa elimu ya juu katika fani mbalimbali ili kufikia kuwa watendaji wazuri wa kimataifa katika uandaaji wa miradi.

Jicho katika kazi za IDC robo ya tatu

Tafiti katika Nyanja za kisiasa- Nigeria

IDC ilimsaidia mgombea ugavana wa mwaka 2015 katika jimbo la Port Harcourt’s kuandaa taarifa ya hali ya kisiasa na utawala bora katika jimbo kutokana na hisia za wapiga kura na wadau wa siasa. Mambo kadhaa yaliainishwa ikiwa ni pamoja na sababu zinazo muongoza mpiga kura kumchagua mgombea fulani,utendaji wa serikali za mitaa kutokana na hisia za watu na hali halisi, matumaini katika serikali mpya na vikwazo katika utaji huduma.

One on one Interview

Wakazi, watumishi wa uma na asasi za kiraia wapatao 1187 kutoka katika serikali za mitaa zote 23 walihojiwa. Timu ya watafiti 11 iliongozwa na mshauri mtaalamu Bankole Allibay pamoja naTema bridge1 meneja wa ofisi Ritha Mboneko wote kutoka IDC. Ilifanya utafiti huu.Katika tafiti hii jumla ya maswali 472 yaliulizwa na takribani matokeo 3000 ya utafiti huo yaliweza kukusanywa kwa pamoja. Mengi ya maswali hayo yaliulizwa kwa mtindo wa maoni,maelezo na ushauri uliifanya IDC kuweza kufikia taarifa zote zilizokuwa zinahitajika kwa kina zaidi na kuleta maana halisi iliyokusudiwa katika tafiti hiyo.Ripoti iliyoandikwa na IDC imepongezwa kuwa tafiti ya aina yake kutokea katika jimbo la Rivers State.

Mbinu ya IDC

1. Ushirikishaji Jamii

Community Meeting, Tanzania

Tunaamini kushirikisha jamii nzima, viongozi, vijana, wanawake, watoto na makundi maalum ni muhimu katika kuunda njia za kuilinda jamii itakayo athiriwa na mradi

 

 

2. Ukweli na Uwazi

ibrah

Tafiti za awali ndio msingi wa kazi za maendeleo, nia ni kuonesha hali halisi. Kila mara tumekuwa tukisimamia ukweli, uwazi na kutoa taarifa bila upendeleo kuwapatia wateja wetu hata kama wasingependa kuzisikia lakini ni muhimu katika kuandaa mbinu mahususi.

 

3. Kutanua fursa kupitia ujuzi wa wenyeji

IMG_0053 (640x360)

Ukosefu wa taarifa unaweza kuzuia jamii kufaidi fursa zilizopo kwenye afya, ajira, mafunzo, elimu na biashara zinazotolewa na serikali za mitaa au serikali kuu, taasisi za kimataifa au NGOs. IDC inawaunganisha watu na miradi mbalimbali.

 

Mbinu za IDC: Utafutaji na usimamizi wa taarifa

1. Tafiti bora

Usimamizi wa taarifa nyingi za kitafiti unahitaji uzoefu, mipango na ujuzi. Kufanya tafiti za msingi za kijamii na kiuchumi, tathmini za athari, tunashirikiana na jamii mbali mbali kubuni mipango yao wenyewe ya wanavyotaka maisha yawe baadaye.

Kwa miaka mingi IDC Ltd imekuwa ikiboresha mbinu zake za kutafuta taarifa za maandishi, picha na taarifa za nyingine zinazokusanywa na timu yetu kila siku. Hususani kubuni njia za kuhifadhi taarifa na kuwezesha kutoa tathmini itakayowezesha kubuni mbinu za kuzuia.

2. Mbinu za tafiti za kijamii

IDC inatumia njia tofauti tofauti kupata taarifa za mbali inazotumia katika tafiti za msingi za kijamii. Mbinu hizi ni pamoja na:

DSC05978 (640x480)

 

 

 

 

 • Tafiti za kina
 • Majadiliano ya vikundi
 • Mbinu shirikishi
 • Upatikaji wa huduma za kiafya na utambuzi wa makundi maalum.
 • Ufuatiliaji
 • Matembezi ya uchunguzi
 • Maigizo
 • Masuala ya jinsia
 • Kulinganisha taarifa
 • Mahojiano maalum

 

Case Study – Huduma za matibabu

P1130476 (640x360)

Upatikanaji wa huduma za afya bado ni changamoto kubwa kwa jamii za kijijini. Kwa kutambua hilo klabu ya Rotary ya Dar es salaam iliandaa kambi ya matibabu, IDC ilisaidia wanakiji watatu kuhudhuria kambi hii. Walipimwa kisukari, shinikizo la damu, malaria, na kupewa ushauri na watalaam.
Bibi Mwanaidi, amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa vikope tangu akiwa msichana. Macho yake yalikuwa yamekwisha haribika lakini upasuaji aliofanyiwa umeondoa kabisa maumivu na kuondoa uwezekano wa kupoteza uwezo wa kuona.

 

Mafunzo ya awali ya sasa yanayoendelea.

Mradi wa mapinduzi ya kilimo cha kijani umekuwa ukichelewa katika utekelezwaji wake pamoja na swala la kufanya uhamishaji wa waathirika wa mradi katika maeneo husika.Hivyo basi IDC imekuwa na mwendelezo wa mafunzo ya awali yanayohusiana na shughuli za kiuchumi ili kuwatayarisha waathirika wa mradi kuwafanya waweze kukabiliana na mabadiliko yatakayotokea katika maisha yao ya baadae.
Mafunzo ya awali kwa waathirika wa mradi ni ya vitendo,gharama nafuu,madhubuti na hufikika kwa upana zaidi kwa jinsia zote na kwa ushiriki wa pamoja.Kozi za mafunzo ya shughuli za kiuchumi ni: 1) Ujuzi wa vitu mbalimbali. 2) Mafunzo ya utambuzi wa fursa na uandaaji wa mchanganuo wa biashara.3) Upataji wa mikopo na 4)Ufuatiliaji endelevu wa kozi ambao umewafanya wengine kuvuka ngazi kubwa katika ufundi wa ushonaji wa nguo.

DSCF93671-150x150.jpg

Ushonaji: Kozi ya awali ilihusu zaidi jinsi ya kutumia cherehani.Kozi ya pili ni upimaji,Ukataji na ubunifu wa mitindo kwa kuanza na ushonaji wa sare za shule. Mafanikio yameonekana na kuweza kuwafanya washiriki waweze kurudisha mkopo wa awali waliopewa.

 

 

EM 4 Carpertery 05-08-2013 (2) (640x480)

Useremala: Waathirika kadhaa wa mradi walihudhuria mafunzo ya useremala katika chuo cha mtakatifu Joseph na kutunukiwa uthibitisho wa hati ya uweredi katika taaluma ya useremala. Mkufunzi alifurahishwa sana na hata kumpatia mwanafunzi mmoja kuajiriwa kuwa mfanyakazi wa kudumu chuoni hapo,Mwingine alivutiwa nae kwa utambuzi wake wa kujua mambo ya ujasiriamali na tayari amesaini nae mkataba ili aweze kupatiwa mkopo ili aweze kuendesha biashara yake mwenyewe binafsi.

 

DSC09744 (480x640)

Kilimo cha urudufishaji/Ubadilishaji: IDC inaendelea kuhamasisha na kuboresha mafunzo ya uboreshaji wa kilimo. Zaidi ya wakulima thelathini (30)walishiriki katika kozi ya utengenezaji wa mboji,kozi hii iliandaliwa kwa lengo la kuboresha mazao ya kilimo.Pili Bakari, ambaye ni mshiriki wa awali katika mafunzo ya kilimo cha bustani na ulimaji wa matunda kwa sasa ameweza kuajiri vijana wawili ambao kazi yao ni kuuza bidhaa zinazotokana na kilimo ambapo huuza kwa wananchi wa vijijini na Safari park hoteli.

 

MIPANGO YA BAADAE:

 • Mafunzo ya kibiashara
 • Uashi
 • Elimu kwa wafugaji
 • Kilimo cha manufaa

 

Wasifu

Ritha Mboneko Meneja wa Ofisi.IMG_20131025_110939_editedNina umri wa miaka 26, mwenyeji wa Kagera, Tanzania. Nimejiunga na IDC toka Desemba 2011 baada ya kuhitimu shahada ya Sayansi ya Kompyuta katika Chuo Kikuu Cha Dodoma
Baada ya muda wa majaribio, kwa sasa mimi ni Meneja wa Ofisi. Naratibu kazi za timu ya ofisini za kila siku, Nasimamia data/taarifa zote za kiofisi pamoja na nyenzo za utafiti zilizotengenezwa kwa ajili ya programu zetu za uhamishaji pamoja na tafiti za awali. IDC imenipa ujuzi wa uongozi kwa vitendo, uchambuzi wa data/taarifa na kujenga, kuishi na kufanya kazi katika timu. Ninajituma, nina uwezo wa kuwasiliana vyema, na pia nina sifa ya kutumia program ya Excel.
IDC ilinipa nafasi ya kufanya kazi katika jimbo la Rivers State, Nigeria, ambayo kazi yangu ilikua ni kuongoza pamoja nakufundisha timu ya ofisini katika utafiti wa kijamii na kiuchumi mkubwa kutokea katika nchi ya Nigeria. Tulikusanya, kuingiza katika database, na kuchambua taarifa zaidi ya 300,000 yakiwa ni majibu ya mtu mmoja mmoja.
Nilihusika pia katika uchambuzi yakinifu, uchoraji wa chati na grafu kwa umahili zaidi ili kuleta maana katika taarifa zilizo katika namba. Mteja wetu aliwasilisha ripoti yetu kwa Gavana wa jimbo hilo na Rais wa Nigeria, Mh. Jonathan Goodluck.Ilikua hatua ya kujivunia katika fani yangu.Imeniongezea uwezo wa kujiamini na kutambua uwezo wangu wa kitaalamu.
Niliporudi Tanzania, nimehusika katika kutengeneza database mpya iliyobuniwa kupokea taarifa za tathimini za fidia za zaidi ya watu 500 walioathirika na mradi mpaka leo na nyingine zaidi zinakuja.
Daniel Ringo Meneja wa Database.1de7f7e
Nimekulia mji wa Old Moshi, Kilimanjaro, nina shahada ya usimamizi wa fedha na biashara. Nilianza kufanya kazi na IDC kama msimamizi wa database na tathimini.
IDC imekuwa ni sehemu muhimu kwa kwa mafunzo, nimejifunza mambo mengi hasa usimamizi wa data na fedha, tafiti kwa kanuni za kimataifa. Zaidi ya haya nimejifunza maana halisi ya kufanya kazi kwa ushirikiano kama timu na kuondoa aibu. Imekuwa ni mwanzo mzuri kwa maisha yangu ya kazi.
Hivi karibuni tumepiga hatua mbele katika kazi zetu . Kwa kutambua vikwazo vya serikali na uhaba wa rasilimali na umuhimu wa jamii kuelewa mchanganuo wa fidia , nilivutiwa kujifunza program ya Microsoft Access ili kutengeneza.mfumo rahisi na unaoleweka wa kutunza data. Kwa kuvutiwa serikali iliomba kutumia mfumo huu katika kuboresha mfumo wake wa uthamini.
Najivunia sana haya mafanikio ambayo nisingeweza kuyafikia bila ushirikiano wa mfanya kazi mwenzangu, Ritha Mboneko.