Tanzania Newsletter June 2013 Swahili Version

Slide01

  

Wafugaji na uhamishaji Tanzania?

Ni kawaida kwa miradi mikubwa ya kilimo inapofika kuanzisha mashamba kuwaondoa wafugaji wanaohama hama bila msaada wowote kwakuwa wanaonekana kama hawamiliki ardhi ila wanaitumia kwa muda tu.

Tangu 2011, IDC imekuwa ikifanya kazi ya Mpango wa Utekelezaji wa Uhamishaji wa Bagamoyo EcoEnergy nchini Tanzania. Tumekuwa tukijihusisha na wafugaji wa ki-Barbaig kwa kipindi chote hicho, tumeendelea kujijengea uaminifu na heshima kwa viongozi, wanawake na vijana kwa pamoja.

Wafugaji wa ki-Barbaig wako katika hali hatarishi na wana changamoto ya kutafuta ardhi kwa ajili ya mifugo yao. Kutokana na wachache wao kuzungumza lugha ya kiswahili, na hakuna aliyeenda shule katika eneo lao, wanahitaji msaada wa kutosha.

Awali mawasiliano na wabarbaig kwenye eneo la mradi yalikuwa magumu kutokana lugha na uzoefu wao wa awali ambao unaowaonesha kuwa mahusiano na wageni yalisababisha wao kuondolewa kwenye ardhi yao.

Mr Shushuda and a pastoralist family
Mr Shushuda na familia ya kifugaji

Afisa wa wilaya kutoka Hanang, Bwana Shushuda ambaye pia ni mfugaji wa kibarbaig alisaidia kuanzisha mikutano ya awali na kuwataarifu kuhusu mradi na haja ya wao kuondoka kwenye eneo la mradi. Mkutano wa kwanza uliwapa wazee wa Kibarbaig fursa ya kutoa madukuduku, matumaini na vipaumbele vyao.

Waliomba mambo matatu:

  1. Wabakiziwe ardhi ndani ya eneo la mradi
  2. Upatikanaji wa madawa ya mifugo
  3. Elimu kwa watoto wao.

Tumeendelea kufanya kazi na wafugaji wa kibarbaig tokamuda huo, na taratibu tumeendelea kujijengea uaminifu na heshima kwa viongozi, wanawake na vijana baada ya kuanza kutekeleza maombi yao.

1. Upatikanaji wa Ardhi

Eneo la mradi wa Ecoenergy lina ukubwa wa hekta 20,000, kwakuwa si eneo lote linafaa kwa kilimo cha miwa, familia 11 zinazozunguka ndani ya eneo la mradi zimekubaliwa kubaki ndani ya hekta 2400 na kutumia mabwawa mawili. Kwa wale wanaotumia mabwawa kwa msimu umetengenezwa utaratibu wa kutengeneza mbauti inayotosha kunywesha ngo’mbe 120 kwa wakati. Pia josho lilopo litakarabatiwa.

Vijana wa kiume wa kibarbaig wamenyakua fursa ya kutafuta ardhi ya kufugia, wametembelea ranchi ya Ruvu kwa ziara ya mafunzo iliyotilia mkazo uchangaji kwenye eneo dogo. Walijifunza kupata ardhi kwenye ranchi inawabidi waanzishe chama cha ushirika. Walirudi na shauku kubwa na kwa kushirikiana na IDC wamefanikiwa kusajili chama chao cha ushirika ambacho ni cha kwanza cha wabarbaig katika mkoa wote wa Pwani.

2. Huduma za Mifugo

IDC waliandaa kikao na Afisa mifugo wa wilaya ambaye alikuwa hajatambua kuwa ng’ombe  katika eneo hilo wanamilikiwa na wabarbaig. Akawashauri kwamba ili wawe wanapata huduma inabidi wajisajiri katika kijiji. IDC Waliwasaidia katika usajili katika  vijiji vya(Fukayosi na Kidomole). Wabarbaig walisema kuwa vijiji hivi vinaongozwa na maadui wao wao wakiasili ,Wamasai, na walikataa kuwasajili. Miezi sita baadae baada ya kufuatila na maongezi ya kina makubaliano yalifikiwa na usajili ukakamilika. Sasa wamesajiliwa, na wanaweza kupata madawa kutoka uongozi wa wilaya.

3. Elimu 

IDC  waliwezesha kufanyika kwa kikao na  Afisa wa Elimu ambaye aliahidi kusaidia katika upatikanaji wa elimu kwa watoto wa Kibarbaig. Hata hivyo viongozi wa Kibarbaig walisema kizuizi kikubwa ni ng’ombe ambao huwa wanahama mara kwa mara ili kutafuta malisho na mabwawa. Mmoja kati ya timu ya IDC anaehusika na wafugaji alishauri kwamba  maeneo ya Hanang walijenga shule ya bweni ambayo ikatatua tatizo hili. Baada ya majadiliano ya zaidi ya miezi 12, IDC ilisaidia  wafugaji kupata kibali cha serikali kuifanya shule ya msingi Bigilo huko Makurunge kuwa shule ya kwanza ya bweni katika mkoa wa Pwani. Fedha inatafutwa kutoka serikalini ili kusaidia ujengaji wa shule hiyo. Wakati huo timu ya IDC imeanzisha elimu kwa watoto ,ili kujifunza msingi wa Kiswahili ,kusoma na kuhesabu. EcoEnergy wamejitolea katika kutoa msaada  kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi kama sehemu ya Mpango wa Uhamishaji Watu(RAP)

A cattle trough in the making
Ujenzi wa mbauti ukiendelea

Fukayosi Mbauti

Kuboresha upatikanaji wa  maji kwa ajili ya mifugo. Afisa  Tekinolojia  wa sanifu wa IDC  Bwana Kizito Mwati akishirikiana  pamoja  na  mhandisi  wa wilaya kujenga  mbauti  kwa ajili ya mifugo ya wamasai na wabarbaig. Wafugaji wa kimasai na kibarbaig  wanafanya kazi kwa  kushirikiana na wakulima kujenga msingi wa mbauti na kusafisha eneo  ili kusaidia urahisi wa kufikika kwa ngo’mbe na kujenga Mbauti. Huu ni ushirika wa kwanza  kati ya wafugaji wenye hofu. Haya ni mafanikio makubwa na ya kihistoria.

MIPANGO YA BAADAYE:

 • BEE kusafusha bwawa namba tatu katika eneo la mradi ( kabla ya kipindi cha vuli)
 • Usaidizi wa kiufundi ili kutengeneza mitaro ambayo itatenganisha eneo la mradi kutoka kwa wafugaji,lengo ni kuongeza upatikanaji wa maji(Mpango wa Dec,2013)
 • Josho la mifugo katika eneo la mradi
 • Hekari 400 za majaribio ya ufugaji wa kutohamahama katika eneo la mradi
 • Kusadia upatikanaji huduma za kisheria katika manunuzi ya ardhi(Inaendelea)
 • Kuendeleza ujuzi zaidi na safari za kimafunzo
 • Utetezi kupitia msaada kutoka IDC NGO-The HELP Faundation

  

IDC Team Profiles

Gelga

Gelga Dakajani, IDC Pastoralist Co-ordinator

Nina miaka  29 nimetokea  katika mkoa wa manyara,Tanzania, na nina stashahada katika mambo ya ufugaji na kilimo. Kazi yangu ni kutafuta ufumbuzi wa matatizo yaliyoelezewa kwenye mazungumzo ya pamoja na wafugaji. Tumewawezesha kufanya usajili wa wafugaji wa ki-barbaig katika vijiji vinavyoongozwa na wamasai, maadui wa jadi wa wabarbaig. Leo hii, vikundi vyote vya wafugaji vinafanya kazi pamoja kwa kushirikiana na timu ya IDC. Haya ni mafanikio makubwa sana. IDC imenielimisha maswala ya uongozi, ujuzi wa usimamizi, afya, usuluhishi, lugha na uandishi wa ripoti, ushauri kwa jamii na uelewa wa uhamishaji kwa kufuata kanuni bora za kimataifa. Ninajiamini katika uwezo wangu wa kupanga, kuendeleza na kufanya kazi na watu wangu kwa malengo yajayo bila kupoteza mila au desturi zetu.

Margareth

Margareth Maina IDC Pastoralist Co-ordinator.

Nina miaka 32, natokea wilaya ya Hanang nchini Tanzania. Nilijiunga na IDC mwezi wa kwanza mwaka 2012. Majukumu yangu hapa IDC ni mwalimu na mkufunzi, nimebobea kwenye usomaji na kuhesabu, afya ya wanawake, na kusaidia biashara kwa wanawake. Kwakuwa binafsi natokea jamii ya wafugaji, nilihusika kwenye masuala ya wafugaji hasa kuwaunganisha na kutafsiria kwa maafisa wa afya na elimu wa  wilaya pia mkuu wa wilaya. Kwa upande wa mafunzo ya hatua za awali, nilikuwa katika nafasi muhimu ya kuwashauri wasichana, kusimamia mafunzo ya upishi na ushonaji. Ninatumia nyimbo na maigizo kama njia ya mawasiliano. Mafunzo yanayotolewa na IDC yameniongezea uwezo wa kuandika, kuelewa shughuli zenye kuleta matokeo, kumaliza kazi kwa wakati na kuandaa michanganuo na bajeti. Pia nimejifunza kutumia program za excel na kuinua mbinu zangu za kusimamia na kutathimini. Pia nimejifunza kutambua uwezo na mapungufu kitu ambacho kimenijengea kujiamini. Fursa ya kuweza kuwasaidia watu wangu wabarbaig kwa vitendo. Ninatamani kuzidi kutumia uzoefu huu kuendelea kufanya kazi na jamii kwenye masuala ya maendeleo, kuwainua makundi yaishio katika mazingira hatarishi na kuwa mtetezi wa haki za wabarbaig.