Tanzania Newsletter December 2013 – Swahili


Utangulizi

IDC Ltd ni mkusanyiko wa wataalamu washauri katika maendeleo endelevu. Tumebobea katika tafiti za kijamii na kiuchumi, Tathimini za athari (ESHIAs), uandaaji wa sera, usimamizi wa utekelezaji, mpango wa makazi mapya (RAPs), Maudhui ya wenyeji na maendeleo ya shughuli za kiuchumi. Tunatumia njia za kibunifu katika kutafuta ufumbuzi wa kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Ingawa tumejikita zaidi Afrika kazi zetu zimeenea kimataifa. Utendaji wa kazi za IDC Ltd unazingatia kuwa endelevu. Tunajenga uwezo wa vijana wahitimu wa elimu ya juu katika fani mbalimbali ili kufikia kuwa watendaji wazuri wa kimataifa katika uandaaji wa miradi.

Jicho katika kazi za IDC robo ya nne

Miradi ya maendeleo hufanya uharibifu zaidi kuliko faida …Isipokuwa

Kuna hisia potofu kuwa miradi inaweza kuchochea maendeleo katika eneo na kuwanufaisha wakazi wa eneo hilo. Ingawa ni kweli serikali inaweza kuongeza mapato kwa kupitia kodi, lakini bila ya kuwa na sera mahususi zinazolenga kusaidia makampuni ya wazawa na kuendeleza ujuzi wa wazawa miradi hii haiwezi kuzinufaisha jamii.

Mara nyingi wawekezaji, wakandarasi huwa na watu wao,hujulikana kama wakandarasi wadogo wenye ujuzi katika fani husika na BZ Child (26)hata wasio na ujuzi hujanao kutoka nje ya nchi.Hii inazuia makampuni ya ndani pamoja na wazawa kunufaika na miradi hiyo. Kuingia kwingi kwa wafayakazi kutoka nje ya nchi husababisha kupanda kwa bei za bidhaa na kushuka thamani ya fedha. Hii inasabisha wananchi kuuziwa bidhaa kwa bei ghali na kudorora kwa uchumi wa nchi, Wazawa hushindwa hata katika ushindani wa kuuza bidhaa ndogondogo na huduma za kawaida katika jamii.

Pia bila ya kuwa na taratibu na kanuni zinazohusu mazingira katika utekelezwaji na ufuatiliaji wake,madhara katika mazingira yatakuwa makubwa katika shughuli mbalimbali za kijamii, zaidi katika shughuli za kijamii na afya kwa ujumla.

Hadi hapo…. madhara yatakapobainishwa na mipango ya kuepusha kuandaliwa kwa kushirikisha wadau ili kupunguza madhara na kutumia fursa mpya
Kuhakikisha hilo IDC inafanya hatua sita shirikishi ambazo ni pamoja na

1. Mapitio ya sheria za nchi, miongozo ya kimataifa na utambuzi wa wadau

2. Utafiti wa kijamii na kiuchumi kwa maeneo yanayozunguka mradi

3. Tathimini ya madhara ya mradi

4. Kuandaa mipango ya usimamizi

5. Makubaliano ya utekelezaji pamoja na kazi za wadau husika,majukumu,bajeti na muda maalumu wa utekelezwaji wake. Ufuatiliaji na Tathimini unahitajika kufanywa na kila mdau ili kuhakikisha kuwa mipango iliyopangwa inafanya kazi,na kufanyiwa marekebisho kwa kadri itakavyohitajika. Mipango mikakati inajumuisha yafuatayo bila ya kuwa na mipaka katika:

Mikakati inaweza kuwa ya masuala mtambuko au yanayojitegemea na inaweza kujumuisha mambo yafuatayo au zaidi:

 • Usalama
 • Usalama katika chakula
 • Muundo wa utawala
 • Nyumba za wafanyakazi.
 • Upatikanaji wa kazi na mikataba.
 • Uhifadhi wa mazingira
 • Maendeleo ya jamii
 • Madhara ya kiafya na magonjwa ya zinaa.
 • Usimamizi wa mazingira
 • Mipango wa usimamizi wa usalama barabarani
 • Madhara katika mahusiano ya jamii.
 • Msongamano katika huduma za kijamii.
 • Mafunzo ya kibiashara
 • Uashi
 • Elimu kwa wafugaji
 • Kilimo cha manufaa

Mbinu ya IDC: Kuendeleza wazawa

Eneo muhimu katika maendeleo endelevu ni kwa wawekezaji wa kigeni kuweza kuwafaidisha wazawa kuongeza mapato. Kuendeleza wazawa ni shabaha muhimu katika utendaji wa IDC. Timu ya wafanyakazi wetu inaundwa na wahitimu wa vyuo vikuu kutoka maeneo tunayofanyia kazi.

Uhamaji mkubwa wa wafanyakazi kutoka sehemu moja kwenda nyingine umekuwa ukisababisha ghasia na migogoroP1110806 mbalimbali,sheria na amri za mamlaka husika kwenye maeneo yenye msongamano na uhaba wa huduma za kijamii. Kushuka kwa thamani ya fedha na upandaji wa bidhaa hauepukiki,ambao husababisha ughali na usalama wa chakula na bidhaa nyenginezo kuwa ghali na katika hali isiyoridhisha.

DSC03752Ubadilishaji wa maarifa kutoka kwa wafanyakazi wetu wakigeni wanaowafundisha vijana wazawa kuhusu masuala ya maendeleo endelevu. Wafanyakazi wakigeni wanajifunza jinsi ya kutumia nadharia pana kwenye maeneo husika. Uhusiano huu unalenga kujenga maarifa na shauku baada ya mradi kumalizika.

 

Mchakato bado unaendelea:Mwendelezo wa taarifa za awali

Miradi kuchelewa si jambo geni, ni dalili ya ugumu wa majadiliano na serikali pamoja mabenki ya kimaifa katika kufikia makubaliano. Mzigo mkubwa wa madhara haya hubebwa na waliochini ambao maisha yao yamesimamishwa. Ucheleweshaji huu unaweza kudhibitiwa.

Bozi trading training (88)
Utendaji bora inamaanisha kuendelea kuihusisha jamii na kutumia muda huu wa ucheleweshaji kuijengea uwezo. Tukiendelea na uhamishaji katika mradi Tanzania, IDC imewezesha duru nyingine ya mafunzo ya shughuli za uchumi. Mafunzo haya yalilenga katika maeneo yaliyotolewa mashaka na wanajamii katika mikutano mbali mbali hasa biashara na usalama wa chakula.

Hadi sasa watu 27 wamepatiwa mafunzo ya kuendesha biashara kuanzia utafutaji masoko, kupima wazo la biashara kwa kuandika michanganuo ya biashara, kufanya tathimini za vizuizi, na kusaidiwa kufanya wazo lao kuwa hai. Hii imepokelewa vizuri na jamii nyingine zimeomba kushiriki.DSC09740

Kutokana na kuongezeka kwa mafuriko na ukame kaya nyingi zinahitaji kupanga uzalishaji wao wa chakula kwa mwaka. IDC kwa kushirikiana na idara ya kilimo halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo iliendesha mafunzo ya jinsi ya umuhimu wa mazao ya chakula na matumizi sahihi ya ardhi. Mafunzo haya yanaendana na usisitizaji mbinu za kuzuia mafuriko ambazo wilaya ilizitumia sehemu nyingine.

 

Shauku ya kutimiza viwango vya kimataifa

Kuna wakati waathirika wa mradi wanahitaji kulindwa japo kuwa wanachokifanya kinaweza kuwa sio sahihi machoni kwa wengi. Fikiria makahaba wanaotegemea biashara kwenye mji unaotarajiwa kuhamishwa kwa malengo ya kimaendeleo. Ataachwa DSCF2242kwenye hali ya mashaka sawa na wengine watakao hamishwa bila kujali anapataje mkate wake wa siku. Hii haina maana kuwa shughuli zinazofanywa kinyume na sheria zinapaswa kurejeshwa baada ya uhamishaji. Lakini uhamishaji unatoa fursa ya kuboresha maisha kupitia mafunzo ya ujuzi na ajira anuai kwa maendeleo endelevu.

IDC ilipata changamoto inayofanana na hiyo kwenye uhamishaji wa wakata mkaa hapa Tanzania. Hawa ni watu wenye kufanya kazi kwenye mazingira magumu, wakiteseka na joto kwa ujira wa pesa. Lakini bado kuna utata kisheria ambapo mara kadhaa polisi wamekuwa wakiwaondoa wanaofanya kazi hizi. Kwa kuzingatia kuwa hili ni kundi lenye hali tete, IDC iliomba kinga kwa waliosajililiwa wasiondolewe. Baada IMG-20140227-WA0010ya kufanikiwa hilo mafunzo ya msingi na msaada kujipanga upya ulitolewa.

Wale waliobaki na kuonesha juhudi walipatiwa ajira kwenye mradi. Hii imewaondoa kwenye ya hatari kufanya kazi kwa kipato kidogo hadi kwenye ajira rasmi. Wamepatiwa mafunzo ya uwajibikaji kazini, usalama kazini na kwa sasa wanaendelea kufanya kazi kwa mafanikio. Huu ni mfano hai wa utendaji sahihi unaonesha jinsi mradi unaweza kuwa na faida zaidi ya uharibifu.

Deogratias Mruah
Mtaalam mshauri – mwandamiziIMG-20140415-WA0007
Natokea mkoa wa Tabora. Elimu yangu ya shahada ya kwanza katika sosholojia kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, imenisaidia kuibua shauku ya kufanya kazi za maendeleo ya jamii. Pia nimefanya kazi na asasi za kiraia katika ngazi ya jamii hadi taifa.
Baada ya kujiunga na IDC mwezi wa tisa mwaka 2011 kama afisa nilipata mafunzo kabambe katika masharti ya uhamishaji kwa mujibu mashirika ya fedha ya kimaifa. Nimebobea katika tafiti za upimaji na ubora, ukusanyaji wa taarifa, kufanya mjidala na tafiti za msingi za kiuchumi na kijamii
Tunafanya kazi kama timu, kila mmoja wetu anaongoza shughuli tofauti. Kama kiongozi wa timu jukumu langu kuu ni kuratibu mawasiliano na jamii na kuongoza tafiti za kiuchumi na kijamii. Nafanya kazi na makundi mbalimbali ya jamii za wafugaji, wachoma mkaa, wakulima na wavuvi. Najihisi ni mwenye bahati kufanya kazi na kampuni ya IDC. Mbinu zetu hususan kutumia uzoefu wa wenyeji zimepongezwa na shirika la maendeleo la Sweden (SIDA)
Ibrahim Bakari
Mtaalam mshauri – mwandamiziOFF Team at Work, 18-05-12
Nimehitimu elimu yangu ya shahada ya kwanza katika fani ya sosholojia kutoka chuo kikuu cha Dodoma.Nilianza kufanya kazi na jumuia umoja wa mataifa Tanzania (UNA). Ndipo nikajiunga na timu ya kampuni ya IDC katika zoezi la hesabu za watu na mali na tafiti za kijamii na kiuchumi katika uhamishaji wa watu kwenje mradi wa Bagamoyo Ecoenergy.
Shauku yangu katika masuala ya afya ya jamii iliibuka nilipoongoza zoezi la upimaji afya liliofanywa na taasisi ya utafiti ya afya Ifakara. Zoezi hili limefuatiwa na tiba na ushauri kwa walioathirika na magonjwa kama vile kifua kikuu,matende,ngiri maji pamoja na ukimwi. Hatimaye nilipanda cheo na kuwa mshauri mwandamizi nikiongoza mahusiano na serikali za mitaa na ushiriki wa wadau.
Kupitia mpango wa utekelezaji wa uhamasishaji, IDC ilitoa mafunzo mbalimbali ya uongozi na usimamizi, utendaji wa kimataifa, mbinu za uwasilishaji, afya na usalama, uandishi wa ripoti na uhusiano wa jamii. Nina uzoefu wa kufanya kazi na viongozi wa ngazi za juu kitu kitakachonisaidia hapo baadaye kushiriki kikamilifu kwenye kuleta maendeleo kwa nchi yangu.