Q1 Newsletter March 2015 – Swahili

  

Hatua za awali ni zipi?

Ni kawaida kwa miradi mikubwa ya kilimo kuchelewesha utekelezaji wa mpango wa uhamishaji. Kipindi hiki ni muafaka kwa hatua za awali zinazolenga kuwaandaa watakao hamishwa na mradi kukabiliana na changamoto za kuhamishwa pia kuboresha maisha yao. Mafunzo ya awali yamedhamilia kuwa ya vitendo na gharama nafuu. Mafunzo haya yamepangwa kuwafikia wengi kujali mahitaji ya kijinsia na gharama ndogo za uendeshaji. Wakati ikiandaa mpango wa utekelezaji wa uhamishaji kwa mradi wa Ecoenergy mwaka 2012

IDC iliwezesha kufanya hatua za awali zifuatazo:

 • Mafunzo ya msingi wa kusoma, kuandika, kuhesabu na ujasiriamali;
 • Elimu ya mazingira kwa jamii wenyeji ya Matipwili  pia  programu za shule;
 • Upimaji wa afya kwa maradhi ya kifua kikuu, malaria, minyoo, VVU, ambapo matibabu yalitolewa kwa wale waliokutwa na maradhi hayo ikiwa ni pamoja na matibabu ya bure kutoka kituo cha tafiti za tiba Ifakara, serikali na Swiss TPH;
 • Matumizi ya umeme jua.

Hii imepokewa vizuri na kuifanya IDC mshirika anayeaminika kwa jamii, imetoa fursa kwa IDC kuanzisha mafunzo ya shughuli za kiuchumi.

Mafunzo ya Shughuli za Kiuchumi

Mafunzo yalilenga kuinua ujuzi na mara nyingine kuongeza vionjo vya biashara ambapo vikundi vinaweza kuundwa na kuanzisha biashara. IDC kwa ufadhili wa Ecoenergy iliendesha mafunzo aina nne kila mwezi kama majaribio kwa mafanikio makubwa. Watu wengi walikuwa na kiwango kidogo cha elimu,  Taasisi nyingi za mafunzo rasmi zilishindwa kusaidia mpango  wa ujuzi wa msingi wa maendeleleo, hata hivyo maofisa wa wilaya, asasi za kiraia na vituo binafsi vilikaribisha fursa hii.kuongeza ushirikiano. Hii iliwezesha uwepo wa majadiliano na wawekezaji wengine katika wilaya.IDC ilitoa mafunzo ya ziada ya vitendo kwa kila ujuzi kwenye jamii. Fursa hii ilianzisha majadiliano na uwazi baina ya kampuni na asasi za kiraia. Washiriki wote wa mafunzo walishiriki katika usimamizi na ufuatiliaji wa mafunzo ili kuboresha yaliyomo kwenye masomo na upokeaji wakati wa utekelezaji kamili wa RAP.Posho ndogo ilitolewa ili watu wote waweze kushiriki mafunzo haya bila kujali kipato. Wanawake wadogo hasa  wale walezi pekee walipatiwa msaada wa ziada ili kuweza kuangalia watoto wao wakati wote wa mafunzo.

Mafanikio ya mafunzo ya awali

Preparing the seedbed
Uandaaji wa kitalu

Hadi kufikia sasa IDC imewezesha mafunzo katika:

 • Ufugaji wa kuku, Upishi, Ushonaji na Udereva
 • Utengenezaji simu, Kilimo cha mboga mboga, Ufugaji wa samaki na Uchomeleaji
 • Uendeshaji wa biashara
 • Uwezeshaji wa vijana na afya bora

Kozi zote ziliambatana na safari za kukuza uelewa kwa biashara zilizofanikiwa kuanzishwa ili kuwatia moyo wanafunzi.

Certificates for caterers
Vyeti vya wapishi

Safari hizi zilijumuisha:

 • Ufugaji kuku Morogoro,
 • Kilimo cha mpunga Bagamoyo na baadhi ya migahawa Bagamoyo,
 • Mafunzo ya udereva Dar es Salaam,
 • Kutembelea ranchi zilizopo mkoa wa Pwani.

Kwa ujumla program za mafunzo zimekuwa za mafanikio makubwa, na kufuatia kuchelewa kuanza kwa mradi, mzunguko mwingine wa mafunzo utaanza hivi karibuniambapo safari hii tutatoa mafunzo ya ujuzi wa hali ya juu zaidi, mafunzo rasmi katika vyuo vya ufundi wa ujenzi pamoja na mafunzo ya upishi yatakayotolewa na mpishi wa timu yetu Patrick.

Kusonga mbele 
IDC inatambua kuwa ujuzi pekee hauwezi kukidhi mahitaji ya jamii, hivyo basi, baada ya mafunzo ya ujuzi, miezi mitatu ya mwisho ya mwaka 2012 na mitatu ya mwanzo ya mwaka 2013 ilitumika kuvisaidia vikundi kuanzishisha biashara. IDC inatambua zaidi ya gharama za kuanzisha biashara inahitajika nguvu za ziada kuwasaidia wale wenye uhitaji wa kujiendeleza kwenye fani nyingine zaidi ya fani za kujikimu. Hii ni pamoja na kuandaa michanganuo ya kibiashara, kusaidia katika kutambua kazi na majukumu ya kila mwanachama, utunzaji wa fedha na kuwekeza faida. Mpango huu unahusisha pia fursa ya mikopo midogo midogo ambayo imeanzisha utamaduni wa kukopa na kulipa ambalo pia ni jambo muhimu hasa wakati wa utekelezaji wa mpango wa uhamishaji.

  Timu ya IDC Sura ya 1

 

Abby

Abigail Mbaligwa

Nina miaka 27 natokea mkoa wa Tabora hapa Tanzania. Kuanzia wakati huo nimehusika kwenye shughuli mbali mbali kama kutafsiri, kiungo kati ya kampuni na serikali na maofisa wa wilaya, kufanya tafiti za kijamii na kiuchumi pia uandishi wa ripoti. Nimefurahia sana muda wangu wa kazi hususan kwa kufanya kazi kwenye jamii ambapo kwa sasa ninaongoza mafunzo ya awali. Nimekuwa nikifanya kazi ya kuchagua washiriki na kutathmini uwezo wa watoa Huduma (Mafunzo). Kufanya kazi na IDC kumenisaidia kujua uwezo wangu wa kujenga mahusiano na uaminifu na watu tunaowafanyia kazi, imenijenga kiakili na kuniendeleza binafsi. Pamoja na changamoto  mbali mbali zimenifanya na uzoefu huu umenipa fursa ya kuona mabadiliko  ya jamii tunazofanya nazo kazi. kuona jamii zikiendeleo ya kijamii na kiuchumi.

 

 

Ushirika wa kuku

Katika hatua za mwanzo kikundi cha ufugaji kuku hakikuweza kufanya vizuri makosa mengi yalitokea. Idadi kubwa ya vifaranga vilikufa kutokana na kucheleweshewa   chanjo na hata wale waliobaki walikuwa na uzito mdogo kutokana na kutokulishwa ipasavyo hivyo kupelekea kuuzwa kwa bei nafuu. Kikundi kilipojitathimini kiliamua kupitia upya kazi na majukumu ya kila mwanachama, waliangalia changamoto na kuja na suluhu zenye kuwafaa. Kikundi pia kilianzisha uhusiano na afisa ugani wa kijiji na kuandaa utaratibu mzima wa ufuatiliaji. Kufuatia hali hii hali ya vifaranga imekuwa nzuri sana.Kwa sasa kuku wanakaribia kuuzwa. Vilinunuliwa vifaranga 114 hadi sasa 102 wamekuwa tena ni wakubwa wapo tayari kwa kuuzwa mapema mwezi juni. Kikundi kimmemchagua afisa masoko na wameanza kupokea oda. Kwa sasa kikundi kina mpangowa kuwa na kuku tayari kwa kuuza kila baada ya miezi minne ambapo watakuwa wanapata faida kubwa. Mafanikio ya kikundi hiki yamekuwa ni gumzo na kuvutia jamii husika,shule za msingi za kawaida na wakazi ambapo sasa vikundi vingine vinakwenda kwao kujifunza jinsi ya kuendesha miradi kwa mafanikio.

  Timu ya IDC Sura ya 2

DSCF2635

Gidufana Gafufen

Nina umri wa miaka 32, asili yangu ni jamii ya wafugaji ya Kibarbagaig wanaotokea wilaya ya Hanang mkoani Manyara. Nina stashahada ya juu katika usimamizi wa biashara na ushirika kutoka chuo cha ushirka na biashara Moshi. Kabla ya kujiunga na IDC nilifanya kazi za ukufunzi wa kujitegemea nikizisaidia asasi za kiraia kuunda ushirika na kutoa mafunzo ya ujasiriamali katika mikoa mitatu hapa nchini.
Hapa IDC nilianza kama ofisa wa mafunzo sio tu kwa wafugaji wa Kibarbaig lakini pia kwa vikundi vya wakulima, wavuvi, na wachoma mkaa. Nilishiriki katika kutoa mafunzo ya ujuzi na ujasiriamali.
Nimeshirikiana na vikundi vyote kuandaa michanganuo ya biashara, usajili na kusaidia kupata mikopo, Sehemu muhimu zaidi ni ufuatiliaji na usimamizi wa vikundi hivi kwa uboreshaji zaidi.
IDC imefanya mafunzo kadhaa ya maendeleo binafsi na kitaaluma, nimejifunza kuhusu taratibu za kimataifa za kuandaa mpango wa utekelezaji wa uhamishaji. Kwa muda niliokuwa na IDC nimeongeza ujuzi wa kompyuta na kwa sasa ninamudu vizuri kutumia program ya excel.
Nimeongeza uwezo wa kuandaa ripoti na kuandaa mipango ya biashara, kuongoza mipango ya kuendeleza biashra ndogo ndogo kumenijenga katika kujiamini.
IDC pia imesaidia uanzishaji wa asasi ya kiraia inayoundwa na vijana wa kifugaji wanne katika timu yetu inayoitwa Help Foundation ambapo tumekuwa tukitoa mafunzo na kuendelea na kazi hii hapo baadae.